Wednesday, 17 August 2016

Timbulo aitaja sababu ya kufuta sauti ya Malaika kwenye wimbo wake mpya

Msanii Timbulo amefunguka sababu iliyomfanya afute sauti ya Malaika na kumweka Nay Lee kwenye wimbo wake mpya wa ‘Ngomani’.

http://hamisishehe.blogspot.com
 
Muimbaji huyo amesema kuwa sababu kubwa iliyosababisha ni kuwa busy kwa Malaika kwa madai ya kutoweza kutokea kwenye video ya wimbo huo kwa sababu zake binafsi.
“Nilimshirikisha Malaika kwenye audio na alifanya vizuri lakini baadaye ilipofika muda wa kushoot video lakini siku hiyo akasema hatoweza kuja kwa sababu zake private,” amemuambia mtangazaji wa Fadhila FM ya Masasi, Dj Magasha.
“Video ilikuwa inahusisha watu wengi na tusingeweza kuisitisha kwa ajili yake tukaamua kumtafuta mtu mwingine aliyefiti kwenye hiyo ambaye ni Nay Lee,” ameongeza.
Aidha Timbulo ameendelea kwa kusema kuwa baada ya kumaliza kushoot video hiyo walirudi studio na wakaamua kuifuta sauti ya Malaika iliyokuwa kwenye wimbo huo na kuingiza upya sauti ya Nay Lee kwa sababu alifanya vizuri zaidi.

Related Posts

Timbulo aitaja sababu ya kufuta sauti ya Malaika kwenye wimbo wake mpya
4/ 5
Oleh

Subscribe via email

Like the post above? Please subscribe to the latest posts directly via email.