Showing posts with label MAPENZI. Show all posts
Showing posts with label MAPENZI. Show all posts

Friday, 12 August 2016

Jinsi Ya Kumuwini Mwanamke Na Mbinu Kumi Za Uhakika

Kujua jinsi ya kumuwin mwanamke si jambo gumu – haswa kama unazijua mbinu za nguvu za kisaikolojia ambazo unaweza kuzitumia kwa mwanamke.


Wanaume wengi wanataka kujua jinsi ya kuwin mioyo ya wanawake na kutaka kujua jinsi ya kuweza kutoka deti na wao. Well, ijapokuwa inaweza kuonekana kuwa jambo gumu, mbinu hizi si ngumu hata kidogo. Mwanzo kama unataka kujua jinsi ya kuwin moyo wa mwanamke kirahisi, basi unapaswa kusoma mbinu kumi ambazo tumeziorodhesha na ambazo hufanya kazi kila wakati.

#1 Approach vile inavyotakikana
Kama unataka kujua jinsi ya kuwin moyo wa mwanamke, kile unachohitajika kufanya ni ufanye mambo ya kibusara tangu mwanzoni. Kufanya mambo yawe rahisi na haraka kwako: weka kwa akili yako kuwa siri ya jinsi ya kumvutia mwanamke yeyote huwa iko kwa dhana anaiyoiweka kuhusu thamana yako kwa akili yake. Kwa urahisi ni kuwa unapaswa kumuonyesha mwanamke kuwa una thamana ya yeye kuweza kuspend muda wake na wewe, na ni yeye ndiye anafaa akuwin na wala si kivingine. Yaani mwanamke anapaswa kukuona kuwa yeye anapaswa kuwa na wewe.

#2 Kuwa tuzo kwa macho yake
Kama tulivyoeleza hapo juu ni kuwa njia rahisi ya kumuwin mwanamke ni kwa kumuonyesha kuwa wewe ni kama tuzo ambalo anapaswa kulishinda na kuwa wewe ni mwanaume ambaye anapaswa kupiganiwa. Kama huelewi hii inamaanisha nini hebu uchukulie huu mfano: kila mtu anajuwa kuwa wanawake wanajichukulia kuwa wao ndio kila kitu ikija kwa maswala ya kutongoza, yaani wao ndio wanaobabaikiwa. Wanajua kuwa pia wanaume kimsingi huwa wanawafukuzia wanawake, ukweli? Well, kama wewe ni mjanja basi unapaswa kufanya kinyume cha haya yote.

Kwa njia nyingine, namaanisha kuwa unapaswa kujeuza akili ya mwanamke unayempenda na kumfanya kuona kuwa ni yeye ndiye anayepaswa kukufukuzia.

Pia unapaswa kumfanya aamini ya kuwa kukupoteza wewe itakuwa ni jambo baya zaidi ambalo atakuwa amefanya katika maisha yake. Hii itahakikisha kuwa hataweza kupoteza interest kwako na atafanya kila kitu kuhakikisha kuwa anakuweka kando yake katika maisha yake.

#3 Ipandishe hadhi yako
Kama unataka kujua jinsi ya kuwashawishi wanawake, unapaswa pia kuipandisha hadhi yako kiujumla mbele za wanawake. Na kwa kuanzia, mwonyeshe kuwa wewe si mwanaume wa tamaa wala mhitaji na hujali iwapo atakukubali au atakukataa. Hii mbinu kiuhakika itamshika kwa mataa kwa kuwa wanaume wengi huwa wanawaangukia wanawake ili kupata atenshen kutoka kwao (wanawake wengi  huwa wanakuwa na mkono wa mbele ikija kwa maswala kama haya.) So, kwa kuchukua hatua ya nyuma, utakuwa unamwonyesha ya kuwa wewe huna tabia kama hio na hii inamfanya kutaka kujua kwa nini wewe ni tofauti na wengine. 
#4 Jenga nguzo na yeye
Njia nyingine ya uhakiki ambayo itaweza kumuwin mwanamke ni kwa kujenga nguzo na yeye. Kimsingi, hapa unaanza kwa kumfanya ajihisi huru na uwepo wako kwa kutumia sanaa za maongezi ya kutongoza. Kwa kufanya hivi, chagua mada ambazo zinamvutia wakati unaongea na yeye na pia hakikisha ya kuwa unampa atenshen zote wakati anapoongea.

Pindi atakapojiskia huru na wewe, unaweza kuanza kujenga mavutio kwa kuanza kumtesa na kumtania mara kwa mara. Lakini, hakikisha kuwa haumuonyeshi kuwa unataka kuwin woyo wake. Mwanzo, itakuwa vizuri zaidi kama utajivuta kwake halafu mwishoni unajitoa mbali na yeye ili uweze kuleta attraction zaidi kati yenu.

#5 Mwonyeshe kuwa unamheshimu
Kama lengo lako kutaka kujua jinsi ya kumuwin mwanamke ni uweze tu kulala na yeye, basi atajua kile ambacho unataka kutimiza kwake na utamfanya akutenge kama jinamizi. Kwa sababu ya hili, unapaswa kumuonyesha kuwa unamheshimu, kivyovyote vile. Kwa lengo lolote lile ambalo unataka kutoka kwa huyo mwanamke, kumheshimu mwanamke kutakufanya uongeze nafasi yako ya kuwin moyo wake mwishoni.

Hii haimaanishi ya kuwa unapaswa kuonekana kama mtu anayeitikia kila kitu kutoka kwake. La. Unapaswa kujua mbinu ya kumtawala pia – kuwa kiongozi na mwenye kudhibiti.

#6 Mwonyeshe kuwa unajali
Kando na kuwa unamheshimu, wanawake wote huwa wanataka kujaliwa. So kabla ya kutarajia mwanamke akuangukie, unapaswa kumuonyesha kuwa unahisia kwake kwa kuonyesha kuwa wewe ni kiongozi na kuwa wewe ndie unayetawala mahusiano yenu. Kama hutafanya hivi, mwanamke wa ndoto yako hataona umuhimu wa kutoka deti na wewe na hatoona shida ya kuwa na mwingine.

ONYO: Tahadhari usivuke mipaka ya kumuonyesha mwanamke kuwa unamjali sana kwa kuwa anaweza kukuingiza katika ile himaya ya kuwa rafiki yake.

#7 Jiamini
Wanaume wengi wanapata ugumu wa kuelewa jinsi ya kumuwin mwanamke na kumwambia kuwa wanampenda. Well, unapaswa kuhakikisha ya kuwa hautamwambia ya moyoni mwako mpaka ule wakati ambao utakuwa confident ndani yako. Huwa kawaida ni hivi, wanawake wanaweza kujua iwapo uko confident au la, na unaweza kupoteza nafasi ya kumuwin mwanammke kama huyu iwapo utaharibu kila kitu kwa kumuonyesha kuwa unashindwa kujiamini ndani yako. 
#8 Simama kati ya wote
Njia nzuri zaidi ya kuchagua wanawake ni kwa kusimama kati ya wote, Mwanzo, kusimama kati ya wote kunaweza kukufanya umuwin mwanamke haraka sana kwa sababu ndoto za wanawake ni kuwa na mwanaume ambaye ni tofauti na wale wengine. So, kama utamwonyesha talanta yako ambayo hakuna mwingine ambae anayo na akaipenda, unaweza kumfanya akuone kuwa wewe ni spesho na kukupenda mara moja.

Labda inaweza kuwa talanta ya kuimba ama labda talanta ya michezo, chochote kile kitasaidia kukutofautisha na wanaume wengine. Unajua kupiga gita ama uko sawa kucheza pepeta? Mwonyeshe!

#9 Kuwa tofauti
Kwa kuendeleza hapo juu, unaweza kutumia hulka yako kuweza kumuwin mwanamke. Kwa kueleza kiurahisi, kuwa na hulka ambayo ni tofauti na mwingine yeyote yule – kuwa na maoni tofauti na ya wale wengine kutakufanya uonekane mtofauti. Njia hii kutamfanya mwanamke kuangalia na kuchagua tabia ambazo ni tofauti na zile za wanaume wa kikawaida. Mara nyingi wanawake waliokomaa kiakili huwa wanawapenda wanaume ambao wako tofauti na wengine.

#10 Badilisha mtizamo wako
Kama unataka kujua jinsi wa kuwin moyo wa mwanamke, basi unahitajika kubadilisha akili yako kabisa – hii ni kuanzia tabia yako, dhana na fikra zako. Pindi utakapofanya hivi, utakuwa na uhakika wa kuwa utawin moyo wa mwanamke wa ndoto yako haraka sana. Njia rahisi ya kubadilisha akili yako ni kujua kuwa kuna myanya mingi unayoweza kuitumia kumuwin mwanamke.

Hatua 6 Za Kumzuzua Mwanamke

Ukweli usemwe. Ndoto ya kila mwanaume katika hii dunia wakati mmoja au mwingine hufikiria kuwa na kipawa cha kuweza kumzuzua mwanamke yeyote anayemzimia. Uzuri ni kuwa hauhitaji kuwa tajiri ama kuvutia ili uwe na kipawa kama hiki.

Kujifunza kuzuzua mwanamke si jambo kubwa vile, mwanzo ni rahisi zaidi kwa mtu yeyote yule kutimiza jambo hili kama atafuata hatua zinazohitajika kwa umakini.

Wengi wa wanaume wanashindwa kumzuzua mwanamke wa ndoto yake kwa sababu wanatumia mbinu ambazo zimepitwa na wakati ama kutumia mitindo ambayo haikubaliki.

Well, nimekuandalia hatua 6 za kufanya ili umzuzue mwanamke yeyote yule.

1. Pokea pongezi
Wanaume wengi wanatabia ya kukataa kupokea pongezi kutoka kwa mwanamke. Balada ya wewe kuguna ama kutojiskia huru wakati mwanamke anakupongeza, mbona usitumie nafasi hii kutumia maneno ya utamu kama ile 'asante, 'nashukuru' nk.

Kupokea pongezi kutoka kwa mwanamke ni kama vile kupokea zawadi kutoka kwake, hivyo kufanya hivi kutakuwa kukimfurahisha mwanamke kila wakati.

2. Kuwa na maoni chanya kujihusu
Kama hujiamini wewe mwenyewe ama unajiona huwezi kutimiza kumfurahisha mwanamke je unatarajia mwanamke akupende? Hivyo basi iwapo unataka kumzuzua mwanamke unafaa ujiamini wewe mwenyewe kama mwanaume.

Njia rahisi ya kutimiza hii ni kuhakikisha unavalia nguo za kupendeza, unavalia marashi yakunukia, na kuwa nadhifu. Wanawake wengi wanapenda mtizamo aina hii.

3. Jifundishe kudensi
Ok wengi wangeuliza kwa nini nijifunze kudensi? Kudensi ina uhusiano wowote upi na kumzuzua mwanamke?
Jibu rahisi. Kwanza ni kuwa wanawake wanapenda sana wanaume ambao wanajua kudensi. Hivi ushajiuliza kwa nini dancers wengi wanapendwa na wanawake?
Pili ni kuwa wanawake wanaamini ya kuwa dancers wengi wanaujua mchezo ikija maswala ya chumbani.
Tatu ni kwa hautarajii mwanamke unayemzimia adensi na wanaume wengine wakati mumeenda kwa kilabu. 

So ni muhimu kujifunza kudensi, atleast style moja mbili za kumdanganya.

4. Tumia jina lake
Siri nyingine ya kumzuzua mwanamke ni kumtaja jina lake wakati wa maongezi. Kulingana na mwandishi maafuru wa kiingereza Dale Carnegie, anadai ya kuwa sauti tamu zaidi kwa sikio la mwanamke ni kusikia ukitaja jina lake.

Kama umekuwa ukifanya uchunguzi ni kuwa wengi wanahepa kutumia majina ya wapenzi wao nk. Hivyo wewe usikubali kuanguka ndani ya hio kategoria. Waonaje sasa uanze kutumia jina lake kila wakati unapomtext ama kuongea naye? Amini usiamini jambo hili linafanya kazi kama uchawi.

5. Muangazie yeye
Iwapo unataka mwanamke akuchukie kwa siku moja basi ongea na kujisifu wewe mara kwa mara wakati mnapoongea pamoja. 

Iwapo unataka kumzuzua mwanamke basi kinachohitajika ni kuhakikisha unampa atenshen yako yote wakati mko pamoja mnaongea.

6. Kuwa mcheshi
Imethibitishwa ya kuwa hakuna mtu angependwa kujihusisha na mtu anayeboa. Hivyo kama unakipawa cha ucheshi ama unauwezo wa kumfanya mwanamke avutiwe nawe basi hio ni silaha kubwa ya kumfanya mwanamke azuzuike kwako. 

Hitimisho: Matumizi ya mbinu hizi na sanaa nyingine za kutongoza tulizichapisha awali zitaksaidia wewe pakubwa kuhakikisha ya kuwa unamzuzua yeyote yule.

Hatua Za Kufanya Kama Mwanamke Hataki Kujibu Texts ZakoUnafukuzia mwanamke mzuri mnaanza kuzungumza. Mnachukua muda wa dakika 20 hadi 30 kuongea na yeye mara ya kwanza. Anapendeza na kuvutia, na unaona kama ni mwanamke ambaye ni yule aliyekuwa ndotoni mwako maishani mwako. Mazungumzo yenu yanaenda vizuri mpaka ukwamwomba namba yake.
Baadaye unajaribu kumtumia text na hazijibu. Labda mnaeza kuchat kwa madakika halafu baada ya hapa anakataa kujibu texts zako. Unabaki ukijiuliza maswali ni kitu gani ambacho umefanya ambacho umekosea. Ok labda anaweza kuwa yupo buzy unampa muda kiasi ajibu text zako...unangojea masaa, siku, wiki mpaka inafikia wakati unagundua kuwa amekupuuza. Kwa nini hajajibu text zako?

So kwa nini hakujibu text zako?
Katika situation nyingi ni kuwa sababu kuu ambayo amekataa kujibu texts zako ni kuwa haukumpendeza mara ya kwanza ulipokutana naye. Ok labda sababu nyingine inaweza ni kuwa ameibiwa simu yake wakati alipokuwa akitext na wewe barabarani ama kitu kingine kama hicho, lakini hapa acha tumakinike na hatua ya kwanza uliokutana naye...yaani first impression ambayo unakudana na mwanamke yeyote.

1. Hakikisha unampendeza mara ya kwanza unapokutana naye
Anaweza kuwa hana muda mrefu wa kukaa na wewe ili akutambue zaidi so kile kitu ambacho unahitaji kufanya ni kuwa lazima uuonyeshe upendo wako kwa kuwa mpole, mkarimu na mtulivu. Hii itamfanya yeye kumakinika na labda kutaka kukufahamu. Hakikisha kuwa wakati unapoongea na yeye tumia mbinu za kuonyesha kuwa ungependa kukutana na yeye wakati mwingine. Kama hakuonyesha dalili zozote za kukuelewa basi hata kama atakupatia namba yake ya simu fahamu ya kwamba itakuwa ni kazi bure. 

2. Taja sababu zako za kuongea na yeye
Mfano: Nimefurahia sana kuongea na wewe. Kusema kweli nimependa maonezi yetu machache. Nataka kwenda lakini naonelea wikendi nitakutext tukutane ili tuongee tena. Hapa utakuwa umeeleza ajenda yako kwake hivyo ukianza kuchat na yeye baadae haitakuwa vigumu kwake kukujibu.

3. Hakikisha kuwa unamtumia text wakati ufaao
Ukiomba namba ya simu kwa mwanamke inamaanisha kuwa wewe umeonyesha intrest kwake vilevile mwanamke akikupatia namba yake ya simu inamaanisha kuwa labda itakuwa amependezwa na wewe. Lakini je, ni muda upi unaotakikana hadi umtext mwanamke huyo.
Wanawake wanapenda kuona wanababaikiwa na kufukuziwa. So usijaribu kumtext hapo hapo wakati amekupatia namba yake. Hakikisha umejibatia shughli nyingi ili usahau kabisa kama uchukua namba kwa mwanamke. Masaa mazuri ambayo yangekuwa sawa ya kumtext ni baada ya masaa 24 baada ya kuchukua namba yake. Hii itamfanya mwanamke yeyote kujiuliza maswali ya kwa nini umechukua muda mrefu kumtext. Itamfanya kuingiwa na maswali ya kama: kwani hajapenda chat yangu? yuko na mwingine? nk. Ukichukua muda huu mrefu hadi kumtext, itakuwa rahisi kwake kukujibi.
ONYO: Hakikisha ya kwamba haupitishi zaidi ya siku tatu kwani anaweza kukusahau kwa haraka ama kuona unampotezea wakati wake.

4. Kitu cha kuandika kwa text yako ya kwanza
Messages za kwanza ambazo utazituma kwa mwanamke zitachangia pakubwa kuona kama wewe uko uko interesting ama unaboa. Unaweza kuuharibu mchezo mzima kama iwapo utaanza kumtext na mambo ambayo hayana manufaa kwake. Kile kitu unachohitajika kufanya hapa ni kuonekana hauna haraka na ujaribu kutumia lugha za kirafiki. Mfano unaweza kujaribu kumtext swala ambalo aliligusia kwa chat iliyopita. Labda aliongea kuhusu kwenda shopping na nduguyake, so swali lakini linaweza kuwa: Je ile shopping yenu na nduguyako iliendaje?. Hii itamfanya kuwa interested na wewe manake ataona ya kuwa ulikuwa umemakinika wakati mlipokuwa pamoja. Hii itamfanya kujibu text zako mara kwa mara bila yeye kuchoshwa.

5. Jaribu kuhepa stori ambazo hazitafikia popote
Mara ya kwanza anaweza kukujibu lakini itafikia pahali atanyamaza. KUMBUKA: Siri kuu ya kumfanya mwanamke ajibu texts zako ni uwe makini kwake, yaani unamtext vtu ambavyo unajua yuko intrested navyo.

6. Weka wazi kuwa unataka mkutano
Acha stori za kumzungusha huku na huku kama wanaume wengine. Ukitaka akujibu text zako hakikisha ya kuwa unadhihirisha azma yako kwa kumwambia kuwa unataka kukutana naye.

7. Usikate tamaa
Kuna wanaume wengine kama wamekataliwa kujibiwa texts zao mara moja basi wanakasirika na wanaachana kabisa na kushungulika tena. Tatizo labda linaweza kuwa mwanamke anakupima akili aone bidii yako kwake. Kama tujuavyo tabia za wanawake ni kuwa hawapendi kuonekana kama ni watu wa kukubaliana na kila kitu hivyo basi wakati mwingine wanakuwa hawaeleweki. 
Ukiona mwanamke amekataa kujibu text yako kwa siku tatu, fanya kumtext tena huku ukionyesha kuwa hauna intrest naye sana vile halafu achana naye. Hii itamfanya yeye kuona una interest na yeye lakini hauna haraka. Baadaye anaweza kuanza chat yeye mwenyewe.

KUMBUKA: Kuna sababu tofauti tofauti ambazo zinaweza kumfanya mwanamke kukataa kujibu texts zako. Labda umemtusi, hujampendeza, ni mwanamke mwenye haya nk. So hizi hatua zitategemea na vile imetokea katika situation 


Mambo Ya Msingi Unapotongoza Mwanamke Katika Kikundi

Kutongoza ni sanaa ambayo inahitaji mmoja kufanya mazoezi ya mara kwa mara ili aweze kuwa na ustadi ambao unaweza kumnufaisha au kumsaidia mhusika wakati ambapo anakabiliwa na tatizo la kumshawishi mwanamke. Ijapokuwa kuzijua sanaa hizi dhidi ya wanawake haitaonekana kuwa na ustaarabu katika jamii, kila mwanaume ana haki ya kuzijua na kutambua mbinu hizi.
Kitu cha kwanza ambacho unapaswa kujua ni kuwa kutongoza si matumizi ya mistari na miondoko ya mwili pekee bali pia ni subira. Kutongoza mwanamke kutachukua muda mwingi kutoka kwako hivyo unahitajika kuwa na imani. Kwa mfano kabla ya kuchukua hatua ya kuapproach mwanamke lazima upime manufaa na hasara ambazo zitakuja iwapo utaamua kutangamana na mwanamke ambae unakusudia kuwa naye.

Ikija swala la kumtongoza mwanamke katika kikundi cha watu, haya hapa ni baadhi ya mambo ambayo unapaswa kuwa nayo wakati unapokabiliana na windo lako.

#1 Kumsifia
Kama umetoka out hadi kwa klabu na marafiki zako halafu ukamwona mwanamke unayemtamani akiwa katika kikundi, muapproach na umuagizie kinywaji na uwe mkweli na mhakika wakati unapomsifia kuhusu umbo lake na nguo alizovalia. Weka katika akili yako kuwa mwanamke anapenda kusifiwa kwa nguo alizovaa, hairstyle yake, macho yake, ucheshi wake na pia marashi aliyoyapaka. Pia, hakikisha kuwa unaspend muda mwingi zaidi hata kama klabu inaenda kufungwa. Kama umeongea na mwanamke huyu usiku huo, hakikisha kuwa unamwambia kuwa umependezwa na kuspend muda na yeye.

#2 Jiamini
Confidence ni nguzo ya kila mwanaume ambayo anapaswa kuwa nayo wakati wowote ule. Mwanaume anayejiamini anatambulika haraka na wanawake. Hivyo lazima uwe na confidence wakati unapotangamana na wanawake. Hii inamaanisha kuwa lazima uonyeshe confidence mbele ya umati na pia uonyeshe kuwa una interest na yeye hata kama umezungukwa na watu. Confidence ni lazima kama unataka kumtongoza mwanamke. Usifikirie sana kuhusu jinsi utakavyompendeza kwa sasa lakini. Kwa kujionyesha wewe mwenyewe bila kujifanya mtu mwingine kutakusaidia zaidi kuliko kuwa muigo wa mtu mwingine ili uonekane mzuri.

#3 Kujieleza
Wakati unapomtongoza mwanamke katika umati, ni bora zaidi kuweka toni ya sauti yako chini na ambayo itavutia kadri uwezavyo. Hii haimaanishi kuwa unapaswa kumnong’onezea, la. Kile unachopaswa ni kuweka wazi sauti yako aisikie vizuri na mara kwa mara umuonyeshe tabasamu ambalo utalichanganya na mvutio wa macho yako. Pia wakati unapoongea onyesha ujuba na maneno unayoyatamka. Hii itamfanya akuone kuwa wewe una interest kwake na unataka kuendeleza aproach yako zaidi.

Wakati utakapokuwa umeuchukua muda wako kuongea na mwanamke na kumuonyesha kuwa uko interested na yeye, jaribu kutafuta ishara ambazo zinaonyesha kuwa pia yeye amevutiwa ama anahisi kama vile unahisi wewe. Ishara hizi utaziangalia kupitia miondoko ya mwili wake. Je anapinda mwili wake upande wako? Je kifua chake amekienua ili uone ukubwa wa matiti yake? Je anacheka mizaha yako hata kama haichekeshi? Kama umeona kuwa amevutiwa na wewe kupitia ishara hizi, basi rudi nyuma na umngojee yeye aanze kuchukua hatua. Hii ni njia hakika ya kumfanya amaintain interest na wewe.

Mambo 15 Mwanamke Huangalia Kabla Kukupenda - Mtizamo Kutoka Kwa Wanawake

Hebu tuseme ukweli, kuna wakati mwingine ambao wanaume wanashindwa kuwaelewa wanawake. Unaweza ukamwaproach mwanamke huku ukijua wazi hutatoboa lakini unashangazwa mwanamke kama huyo anakukubali fasta.

Na wakati mwingine utaapproach mwanamke ambaye unaamini kuwa ni rahisi kabisa kumtongoza lakini ukirusha nyavu badala ya kushika samaki inanasa mawe (sitaki kusema kinachotokea wakati mwanamke anakuzima mbele ya hadhira)

...halafu sasa kuna wale marafiki zetu ambao kila wakati wao wakitongoza wanakataliwa. (inauma sana)

Well, usitie shaka tena coz hivi karibuni kama Nesi Mapenzi tumekuwa tukitafiti kwa kuuliza wanawake ni mambo gani ambayo yanawavutia sana kutoka kwa wanaume na mambo ambayo yanaweza kuwafanya wafall in love na wanaume na haya ndio mambo ambayo waliyazungumzia sana:

#1 Kuvalia nadhifu
Kulingana na wanawake ni kuwa mwanaume anapaswa kuvalia nadhifu kila wakati. Hii ni muhimu kwa mwanaume kwa kuwa huwezi kujua ni wapi au lini unaweza kukutana na mwanamke wa ndoto yako. Ni jambo muhimu la kuzingatia lakini masikitiko ni kuwa ni wanaume wachache ambao huwa wanaona umuhimu ikija katika hili swala. Ok. ni hivi, kuanzia sasa hadi milele hakikisha kuwa unavalia kisafi na kinadhifu wakati wote, jipulize marashi na utumie bidhaa zote za wanaume ambazo zitakupamba.

#2 Kuwa na msimamo
Jambo ambalo wanawake wanachukizwa kutoka kwa wanaume ni kuona mwanaume ambaye hana msimamo thabiti. Mara leo anasema hivi mara siku nyingine yuko hivi. Well, hapa siongei kuhusu mwanaume ambaye mambo yake hayajulikani (mysterious) La. Naongea kuhusu wale wanaume ambao hawawezi kuwa na misimamo yao wenyewe. Akili zao haziwezi kujitegemea, hawezi kusema jambo mpaka aulize ushauri kwa wenzake ama kwa marafiki zake. So kama wewe ni mwanaume ambaye una tabia kama hizi ziache kuanzia sasa. Nataka ujeuke. Ukiwa na tabia kama hii hutatoboa katika kutongoza mwanamke.

#3 Mwanaume mwenye kuvutia
Mwanaume ambaye anajua kuvutia wanawake ni silaha nzito katika sanaa ya kutongoza. Wanawake wanapenda mwanaume yeyote ambaye ana chembechembe za kusisimua wanawake. Na mwanaume kama huyu ni yule ambaye ana uwezo wa kutumia miondoko ya mwili ipasavyo, wale ambao wanajua kutumia sanaa ya kubanta, na wale wanaojua kuzungumza maneno ya kunata. Upo? [Soma: Mbinu za kufuata uonyeshe kuwa una ushawishi]

#4 Mwili mzuri/shepu
Kama vile ambavyo ungependa mwanamke mwenye shepu na figa, pia wanawake wanapenda wanaume wenye shepu. So utafanyaje kama wewe una shepu la duara? Ingia gym, fanya mazoezi ya kukimbia angalau dakika 30 kila siku. Hii itakufanya uwe na toni nzuri kwa mwili wako. Si mimi ndio nimesema hivi, ni maneno kutoka vinywa vya wanawake. Anza mazoezi pindi utakapomaliza kusoma hii post.

#5 Kuwa na sanaa ya ucheshi
Mwanamke anaweza kujua iwapo mwanaume anachembechembe za ucheshi au la wakati ambapo anaongea naye. Ni hivyo tu ambavyo unahitajika kuwa navyo wakati kama unataka kumfurahisha mwanamke. Kila wanawake wanajua kwamba mwanaume ambaye ni mcheshi huwa anavutia sana haswa ikija katika maswala ya kudeti na wakati wanapochat nao kupitia kwa simu. Hivyo jambo lako la kufanya ni hakikisha ya kuwa wakati unapoongea na mwanamke unamchekesha. Usijilazimishe kama wewe si mcheshi. Mwanamke anaweza kucheka kwa mizaha ambayo hata haichekeshi kama umemsoma mambo anayoyapenda.

#6 Mwanaume ambaye halazimishi mambo
Mwanaume ambaye hulazimisha mambo huwa ni wanaume wanaochukiza zaidi ikija katika mchezo wa kudeti. Mwanaume wa kulazimisha ni yule ambaye anakubali kushindwa ili kuzuia mgogoro na mtu ambaye amemshinda kihadhi. Wewe kama mwanaume haupaswi kujidhalilisha mbele ya yeyote yule, hata kama ni marafiki zako. Kuwa na misimamo yako mwenyewe katika maisha yako. Kama unaona kuwa unakosewa una haki ya kupaza sauti yako usikike  balada ya kukasirika ama kusinyaa.

#7 Kazi nzuri na hela ndefu
Ok. Haya si maoni yangu. Ni mambo ambayo yametamkwa kutoka kwa vinywa vya wanawake. Lakini ngoja tuseme ukweli...pesa ni muhimu ikija katika maswala ya mapenzi. Ni hivi! Wewe hupenda wanawake warembo zaidi kuliko wanawake wabovu. Kweli? Hivyo hivyo wanawake hupenda wanaume ambao ni matajiri zaidi kuwaliko wale maskini. Kuwa tajiri na kuendesha gari la kifahari ni advantage kwako (usitie wasiwasi, haya ni maoni ya wanawake tu. hapa Nesi Mapenzi tushalizungumzia tatizo hili mara kwa mara, pesa si muhimu katika kutongoza, ushapu wako ndio muhimu)

#8 Mwanaume ambaye anaheshimiwa na wengine
Wanawake wanapenda wanaume ambao wanawaheshimu, lakini pia wanapenda kuwa na wanaume ambao wanaheshimiwa na wengine. Kama kuna mtu hakuheshima, hayo ni makosa yako? Kama ni yako basi hakikisha kuwa unatatua. Lakini kama si makosa yako basi si lazima ujihusishe nao. Simama wima na utetee haki yako ya kuheshimiwa na kila mtu. Tumeelewana?

#9 Mwanaume anayejiamini
Kuwa na confidence ni muhimu kwa kila mwanaume. Ni nguvu ya kuzimu ambayo kila mtu utakayekutana naye atakuonea gere. Mwanaume anayejiamini huwavutia wanawake kwa kuwa anajiamini yeye mwenyewe pamoja na uwezo wake wa kuyaona mambo jinsi yalivyo ulimwenguni. [Soma: Hatua za kujiamini]

#10 Mwanaume anayeonekana vizuri
Huku ni kuanzia kule kujiweka kimwili. Vile ambavyo unasimama kama mwanaume. Je mapozi yako yakoje? Je unavalia nguo kulingana na mwili wako? Wakati unapoongea unazungumza na ishara zipi? Haya yote ni baadhi ya mambo ambayo  ni muhimu na yanayowafanya wanawake wakutambue kama wewe ni mwanaume bora wa kumchumbia au la.

#11 Mwanaume anayejua kuzungumza
Kama tu vile kujua jinsi ya kutumia ucheshi katika mazungumzo yako, kujua jinsi ya kuzungumza na mwanamke kwa kutumia Sanaa ya Mazungumzo kama vile banta, miondoko ya mwili na kuchanganya Programu ya Isimu Ubongo ni muhimu zaidi kwa kuwa kutamfanya mwanamke kujiskia huru zaidi akiwa na wewe na ni mambo ambayo mwanamke anatamani kutoka kwa mwanaume yeyote. Sanaa zote hizi ziko kwa kitabu cha Kutongoza Mwanamke: Kuanzia Hadharani Hadi Kitandani

#12 Tabia ya kuheshimu
Kuwa na tabia ya kuheshimu wengine vile inavyotakikana. Wanawake wote wazuri hawawapendi wanaume ambao wanapenda kuwachukulia vibaya wengine. Usiwe mbaya kwa watu walioko chini yako bila ya kuwa na sababu yeyote. Ukiheshimu wengine nao pia watakuheshimu. Wanawake huwaona wanaume wenye tabia ya kuwaheshimu wengine kuwa wanaweza kuwa wazazi wazuri. So hakikisha kuwa unatabia nzuri wakati wote.

#13 Kuwa mwanaume alpha
Wanawake wazuri huwa kwa mikono mwa wanaume bora. Hakuna mwanamke atataka kuwa na mwanaume mwoga, asiyejiamini, asiyeheshimu wengine. Itakuwa ushawahi kugundua kitu flani, kwa kawaida huwa kuna mwanaume mmoja katika kikundi flani ambapo yeye anadeti wanawake warembo zaidi ilhali wenzake wanadeti wanawake wa kawaida. Wanaume kama hawa ndio huitwa alpha. [Soma: Hatua za kujijeuza Alpha]

#14 Mfanye ajihisi huru
Wanawake wanapenda wanaume ambao wanawafanya wajihisi huru wakiwa nao. Hii ni kulingana na usemi kutoka kwa wanawake. Hivyo kama wewe unakuwa na tabia za maswali yasioisha, ukali, woga ama kutojiamini basi utamfanya mwanamke ashindwe kujiskia comfortable akiwa na wewe. Jambo la kuhakikisha ni kuwa unautoa wasiwasi wowote ambao unaweza kujitokeza wakati unapoongea na yeye.

#15 Mwanaume mwenye usambamba/ compatibility
Ok. Tatizo kuu linajitokeza hapa. Mara nyingi mwanaume anaweza kumpendeza mwanamke kwa kila kitu lakini mwanamke anaweza asikubali mwitikio wako kwa kuwa hamna uwiano ulio sawa. Mwanamke anaweza kukukataa kwa sababu zake binafsi. Kama unataka kufanikiwa na hili basi hakikisha kuwa unakuwa mkweli, makinika na interests zake na usome mambo anayopenda na kuchukia. Kama ataona kuwa kuna uwiano ndani yenu, basi ni rahisi kwa yeye kukukubali.

Mwisho ni kuwa haya ni maoni ambayo yametoka kwa vinywa vya wanawake, hivyo kama kuna moja kati ya haya maoni 15 tuliyoyaorodhesha unayakosa, basi ni muhimu uanze kazi sasa hivi.

Mafanikio Kwako.

Hatua 3 Za Kufuata Unapomtongoza Mwanamke

Kama unataka kumpata mwanamke unayemzimia bila tatizo lolote basi hakikisha unafuata kila kitu ambacho utasoma sahizi. Hii mbinu imeibwa kutoka kwa kitabu cha Jinsi Ya Kumtongoza Mwanamke: Kuanzia Hadharani Hadi Kitandani - ambacho nakipendekeza kwa yeyote yule ambaye yuko tayari kutumia maujanja ya mazungumzo kumnasa mwanamke yeyote.


Inaenda hivi...

Hatua #1: Angalia ishara.  Ufunguo wa kutongoza ni kuzijua na kuzivumbua ishara fiche kwa yale anayofanya na kutenda. Makinika na stori ambazo anaeleza, mambo ambayo anapenda kuongea na kila kitu ambacho kinaamsha hisia zake. Kumbuka hapa unamakinika na mwanamke na wala si wewe. Usijaribu kutoa maoni  yeyote bila kufikiria madhara yake. Unataka kumtongoza - na hautaki maoni yako yaonekane kama kipingamizi.

Hatua #2: Cheza na hisia zake.  Hapa jambo muhimu la kufahamu ni kuwa - kwa kuchagua mambo yafaayo kumwambia mwanamke, unaweza kubadilisha hisia zake hadi vile unavyotaka wewe. Huu uwezo wa 'kubadilisha' hisia za mwanamke ni jambo MUHIMU zaidi ya yote ikija katika maswala ya kumtongoza mwanamke.

Ingiza hisia nyingi iwezekanavyo katika mazungumzo yako kwake. Jibu stori zake na hisia zifaazo na utakuwa umejitenga mbali na wanaume wa kawaida ambao wanamuapproach.

Hatua #3: Mpe uhakikisho. Kila mwanamke (hata kama ni mrembo kiasi gani ama 'amekamilika' mbele ya macho yako) huwa wanakutojiamini ndani yao ambako kunahitajika kupewa uhakikisho kwa njia moja au nyingine. Hivyo hivyo, jambo muhimu la kuzingatia wakati unampa uhakikisho ni pale ambapo utakuwa mkweli wakati ambapo unampa huo uhakikisho.

Kumwambia kuwa ana macho mazuri hakutasaidia - hii ni kwa sababu maneno kama haya yashatumika mara kwa mara, na kila mwanaume anatumia maneno yayo hayo kama anataka kuingia ndani ya chupi ya mwanamke. Kumpongeza na kumpa uhakikisho kwa jambo ambalo hajiamini nalo kutamfanya akuthamini na kukuweka karibu na yeye zaidi. Na kama umefuata hatua hizi mbili za kwanza vizuri basi hautakosa kupata jambo ambalo litampendeza.

Huu uwezo wa kumtongoza mwanamke kwa kutumia maongezi ni advantage ya kikweli ambayo mwanaume anapaswa kuwa nayo. Ni jambo ambalo ni bora kuwa nalo kama unataka kuwa na nafasi nzuri kwa mwanamke yeyote.

Jinsi Ya Kumpata Mwanamke

Kila mwanaume ashawahi kupenda mwanamke spesho katika maisha yake. Unamjua wewe mwenyewe. Ana hulka ambayo ulipendezwa nayo, ana uso mzuri na nywele za kuvutia. Lakini tatizo ni kuwa anadeti wanaume bora mara nyingi, so utafanyaje mpaka akuone kuwa wewe ni bora pia na umfanye anotice uwepo wako?
Ok, kulingana na maumbile ya wanadamu ni kuwa wanaume huwa wananotice uwepo wa mwanamke kulingana na urembo wake ilhali wanawake wananotice uwepo wa mwanaume wakati hulka yake inang’aa. So, mwanaume bora kwa mwanamke ni Mwanaume Alpha – kiongozi anayejiamini na ambaye anapata kila kitu anachotaka wakati anapotaka. Kuwa Mwanaume Alpha ni njia rahisi kwa mwanamke kukupenda, kwa haraka sana.

Unapotaka kuchukua atenshen ya mwanamke, hakikisha kuwa hauonyeshi tabia ya uhitaji mwingi, bali mwonyeshe kuwa anapaswa kufanyia kazi ili aweze kupata time aspend na wewe. Yaani kwa njia rahisi ni kuwa unapaswa kuonyesha kuwa haujali kama yuko interested na wewe au la. Lakini pia usimfanye afikirie kuwa wewe ni changamoto kwake, bali kuwa changamoto wewe mwenyewe.

Kando na kuweka thamani yako mwenyewe, unapaswa kuipanua himaya yako ya kutangamana na wengine yaani ongeza idadi ya marafiki zako na pia wanawake wengi. Uzuri ni kuwa wanawake ni rahisi kuwa marafiki nao. So hakikisha ya kuwa unatangamana na wengine. Kufanya hivi hakutaongeza thamani yako mbele ya jamii pekee bali pia inakuwa kama kichocheo cha wewe kuweza kuwa na confidence mbele ya wanawake. Pia hakikisha unatoka deti na wanawake wengi kadri iwezavyo. Hii itakupa nafasi ya wewe kujifanyia zoezi ili ile siku utatoka deti na mwanamke unayempenda haitakuwa tatizo kubwa.

Kama mawazo yako yamejikita kwa maneno kama, “Nahitaji kumuwin huyu mwanamke”, “Huyu mwanamke anapaswa kuwa wangu pekeangu”, ama “Siwezi kuacha kumfikiria”, basi jizungushe na wanawake na matatizo ya fikra kama hizi zitakuepuka.

Tena, wakati wanawake wanapowaona wanawake wengine wakitangamana na mwanaume flani, watafanya bidii pia na wao watangamane na mwanaume yuyo huyo. Hii inajulikana kama ithibati ya kutangamana na huwa ina nguvu sana wakati inapotumiwa kwa wanawake. Kama umeshawahi kumuona mwanaume akiandamwa na wanawake wengi, basi hio itakuwa ithibati ya kutangamana kwako.
Sasa, kwa kuwa hakuna tatizo lolote la kuona mwanamke anayevutia na ambaye unahisia na yeye, unapaswa kujikumbusha kuwa kuna wanawake wengine wengi na warembo ambao wanaweza kuwa wazuri kama vile alivyo mwanamke wa ndotoni mwako. Kama utaendelea na kuwa na mawazo ya kuwa mwanamke wa ndotoni mwako hawezi kubadilishwa na mwingine, basi atashikilia nguvu juu yako na mwishowe atapoteza hamu na wewe. Kumbuka – kuwa Mwanaume Alpha. Chukua control katika hali kama hii na utampata bila kupoteza wakati.

Ok, ni vizuri kumwona kuwa ni mwanamke bora, lakini fahamu kuwa kuna wanawake bora zaidi kule nje. Hii itasaidia kuondoa uhitaji mwingi, na kukufanya kuonekana kuwa na thamani na kuweza kumpata mwanamke umemweka ndotoni mwako mwishowe.