Wednesday, 17 August 2016

Darassa adai video ya ‘Too Much’ ilimtoa jasho

Rapper ambaye anafanya vizuri kwa sasa na ngoma yake, ‘Too Much’ Darassa, amesema video ya wimbo huo ilimtoa jasho


http://hamisishehe.blogspot.comAkiongea na kipindi cha Funiko Base cha Radio 5, Darassa alisema imemchukua muda mwingi na pesa nyingi kuikamilisha video hiyo kwakuwa alitaka kufanya kitu kikubwa.
“Too Much kwangu ni video kubwa na imetucost,imetuchukua muda,imetuumiza hapa ninavyoongea hakuna tulichobakiwa nacho zaidi ya nguvu na akili tu,” alisema.
“Tulichokuwa tunataka ni kuhakikisha tunatengeneza video nzuri nyumbani hata tukifanikiwa kimataifa watu wajue jamaa ameendelea tu ila alianzia nyumbani ndio tunachopambania,watu wa nje wahitaji kufanya kazi na sisi.”
Video ya wimbo huo iliongozwa na Hanscana.

Related Posts

Darassa adai video ya ‘Too Much’ ilimtoa jasho
4/ 5
Oleh

Subscribe via email

Like the post above? Please subscribe to the latest posts directly via email.