Friday, 17 November 2017

MSIBA WA NDIKUMANA WAMTESA UWOYA


Staa wa Bongo, Irene Pancras Uwoya.
WAKATI kifo cha aliyekuwa mume wa staa wa sinema za Kibongo, Irene Pancras Uwoya, Hamad Ndikumana Katauti (39), raia wa Rwanda kilichotokea usiku wa kuamkia Jumatano wiki hii, kikiibua utata kutokana na mshtuko wake, hali hiyo kwa mkewe huyo inafananishwa na kile kilichomkuta mwanamama Zarinah Hassan Tiale ‘Zari The Boss Lady’ kwa mumewe, Ivan Ssemwanga ‘Don Ivan’ miezi kadhaa iliyopita.
VYANZO VYA RWANDA
Kwa mujibu wa vyanzo kutoka nchini Rwanda, chanzo cha kifo cha mume wa Uwoya ni matatizo ya moyo huku kikishangaza kwani jana yake (Jumanne) alikuwa fiti akiendelea na kazi zake kama kawaida.
Hadi anakutwa na umauti, Ndikumana alikuwa Kocha Msaidizi wa Timu ya Rayon Sports ya Rwanda ambapo saa kadhaa kabla ya umauti alikuwa akifanya mazoezi na wachezaji wake.
Akithibitisha kutokea kwa kifo hicho, Afisa Habari wa Rayon Sports, Gakwaya Olivier alisema kuwa, Ndikumana alifariki kwa kile kilichosadikiwa kuwa ni ugonjwa wa moyo.
UTATA
Utata wa kifo cha Ndikumana unaelezwa kutokana na namna kifo hicho kilivyotokea ghafla.
“Alisikia maumivu makali kifuani, akaomba soda ya baridi, wakamletea na alipomaliza kunywa kidogo tu, alitapika kisha akaishiwa pumzi na ndipo akakata kauli,” alisema afisa habari huyo.
Akiwa katika pozi.
NDOA YA UWOYA NA DOGO JANJA YATAJWA
Wakati simanzi hiyo ikizua mjadala mkali, baadhi ya watu walidai kuwa, matatizo hayo ya moyo huenda yalitokana na msongo kufuatia mkewe huyo ambaye alikuwa hajampa talaka kudaiwa kufunga ndoa na msanii wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ hivi karibuni.
Wachambuzi wa matukio ya mastaa Bongo walieleza kuwa, baada ya stori za Uwoya na Dogo Janja kuibua mjadala mzito, Ndikumana alikuwa akiposti maneno ya mafumbo mitandaoni kabla ya kumtambulisha mpenzi wake mpya.
UWOYA YAMKUTA YA ZARI
Ilisemekana kwamba, kifo cha mume huyo wa Uwoya kinatengeneza mazingira kama yale ya kifo cha mume wa Zari, Ivan ambaye naye alikutwa na umauti kutokana na matatizo ya moyo na baadaye kufuatiwa na mama yake.
NDIKUMANA KAMA IVAN
“Kifo cha Ivan na chenyewe ilidaiwa kilitokana na msongo baada ya Zari kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mtu mwingine kama ilivyo kwa Ndikumana baada ya Uwoya kudaiwa kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Dogo Janja,”
kilisema chanzo hicho na kuongeza;
“Kilichomkuta Uwoya kinafanana kabisa na kile kilichotokea kwa Zari kwani utagundua kuwa wote waliingia kwenye mapenzi na wasanii wa Bongo Fleva.
Irene Pancras Uwoya na Hamad Ndikumana Katauti (39) enzi wakiwa pamoja.
HAKUKUWA NA TALAKA
“Kama hiyo haitoshi, wote walikuwa hawajapewa talaka na waume zao na hata ugonjwa uliowasababishia waume zao umauti ni ugonjwa wa moyo.
“Pia wote vifo vyao vilikuwa vya ghafla kwani hawakuripotiwa kuwa wanaumwa.
BADO WALIWAHITAJI
“Kibaya zaidi wote walisharipotiwa kuwa wapo kwenye hali mbaya kutokana na kutoswa na wake zao ilihali wakiwa bado wanawahitaji.
“Ivan alikuwa akimbembeleza Zari kumrudia kama ilivyokuwa kwa Ndikumana ambaye miezi
kadhaa iliyopita alikaririwa akisema kuwa, amekuwa akimuomba Uwoya arudi kwake waendelee na maisha hasa katika suala la kumlea mtoto wao wa kiume aitwaye Krish.
Kwa upande wake, Ivan alikutwa na umauti Mei 30, mwaka huu ambapo katika ndoa yake na Zari, walijaliwa watoto watatu wa kiume, Pinto, Didy na Quincy.
MAMA UWOYA AANIKA SIRI
Kwa upande wake mama Uwoya, Naima Uwoya alianika siri ya kushangaza juu ya mwanaye huyo na Ndikumana ambapo alisema kuwa, alihangaika mno kurudisha uhusiano wa wawili hao lakini ikashindikana.
Mama Uwoya alisema kuwa, katika kurejesha ndoa hiyo, alikwenda hadi nchini Israeli kwa ajili ya kufunga na kumuomba Mungu ili wawili hao wamalize tofauti zao na aliamini ipo siku mambo yangekuwa sawa, lakini ndiyo hivyo Mungu naye alikuwa na mipango yake.
MAZISHI YA NDIKUMANA YATIKISA
Ndikumana alizikwa Jumatano iliyopita nchini Rwanda ambapo mazishi yake yalitikisa kutokana na uwepo wa ndugu na marafiki wengi waliojitokeza katika mazishi hayo.
Uwoya alishindwa kwenda kumzika kwa kile kilichoelezwa na watu wake wa karibu kuwa alikuwa jijini Dar na ilikuwa ni ghafla mno hivyo leo (Ijumaa) anatarajiwa kwenda kuhani msiba nyumbani kwa Ndikumana jijini Kigali, Rwanda akiongozana na wasanii wenzake wa Bongo Muvi.
TIMU ALIZOCHEZEA NDIKUMANA
Hadi anakutwa na umauti, Ndikumana aliyezaliwa Oktoba 5, 1978, aliwahi kuzichezea timu mbalimbali zikiwemo Rayon Sports na Timu ya Taifa ya Rwanda kuanzia mwaka 1998 na kuwa nahodha wa muda mrefu wa timu hiyo iitwayo Amavubi.
Pia alicheza soka la kulipwa Ulaya katika Timu za Gent na Anderlecht za Ubelgiji, Omonia Nicosia na Limassol za nchini Cyprus kabla ya kumalizia soka lake la uwanjani akiwa na Stand United ‘Chama la Wana’ ya nchini Tanzania.
TULIKOTOKA
Julai 11, 2009, Ndikumana alifunga ndoa na Uwoya katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph jijini Dar kabla ya ndoa yao kuvunjika rasmi miaka minne iliyopita.

Source: global publishers

HIKI NDO ALICHOANDIKA MANGE KIMAMBI KUHUSU HUKUMU YA LULU

newzzzzzzzz..... Lulu amekutwa na hatia ya kuuwa bila kukusudia na amehukumiwa miaka miwili jela.......
.
.
.
Dah huyu jaji anawaza kama mimi posti yangu niliyoposti masaaa mawili yaliyopita nilisema ningekuwa jaji ningemkuta na hatia ila ningempa adhabu ndogo mwaka mmoja au miwili jela.......
.
.
Jaji ametenda haki....
.
.
Sio kama nimefurahi Lulu kafungwa nilichotaka ni kuona hakuna double standards, nilitaka kuona haki inatendeka. Na Lulu ana deserve hiyo miaka 2 jela labda itampa muda wa kufikiria how her actions affected Mama Kanumba na familia yake. Labda akitoka atakuwa more humble......
.
.
.
Lakini still mwanasheria wa serikali achukulie hatua za nidhamu na afukuzwe kazi!! Alijaribu sana kusabotage kesi ili amsaidie mtuhumiwa......
.
.
PS: December Magu anatoa misamaha kwa wafungwa, sidhani kama atawasahau wafungwa wa kumpa kiki ya kufungia mwaka kama Lulu na kina Babu Seya maana ile barua ya kina Baba Seya had Bashitel written all over it."

Million 900 INAPENDEZA ADATA KWA WEMA SEPETU

BILIONEA wa nyumba za Lugumi, Dkt Louis Shika amemfungukia ‘Tanzania Sweetheart’, Wema Issac Sepetu kuwa ni staa ambaye anamkubali ukiachana na huyo kwa upande wa muziki Ray C ni mmoja wa mwanadada ambaye anamkubali kupitia nyimbo yake ya nataka niwe na wewe

Wednesday, 1 November 2017

LULU AFANYIWA MAOMBI ZIKIWA ZIMESALIA SIKU CHACHE HUKUMU KUTOLEWA


Zikiwa zimesalia siku 12 tu kabla ya hukumu yake kusomwa kufuatia kesi yake ya kuua bila kukusudia inayomkabili, taarifa zinasema maombi na sala zimekua zikitikisa nyumbani kwa msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Mtu wa karibu wa msanii huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake, alilidokeza Risasi Mchanganyiko kuwa, baada ya kesi hiyo kufikia katika hatua ya hukumu, hivi sasa kila siku maombi yanafanyika asubuhi, mchana na jioni, kwani kwa hali ilivyo hivi sasa, kila kitu kimo mikononi mwa Mungu.
HISTORIA YA LULU: Elimu Yake, Alivyokutana na Kanumba, Familia Yake na Kila Kitu Kuhusu Yeye!!!
“Si Lulu, si Mama yake, si ndugu zake, kila mmoja anaomba kwa muda wake, wakati mwingine kwa pamoja, au mmoja mmoja, wanachojua wao hatima ya kila kitu ipo mikononi mwa Mungu, ndiyo maana sala zinaelekezwa kwake,” alisema mtu huyo.
Lulu anashtakiwa kwa kosa la kumuua bila kukusudia, aliyekuwa mpenzi wake, Steven Kanumba, katika tukio lililotokea nyumbani kwa msanii huyo, Sinza Vatican mwaka 2012.
Baada ya kusikilizwa kwa ushahidi wa Jamhuri, upande wa utetezi na wazee wa mahakama, sasa hukumu hiyo itasomwa Novemba 13, mwaka huu katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na Jaji Sam Rumanyika.

PREZOO ADATA KWA AMBER LULU


MWANA-MUZIKI na muuza sura kwenye video mbalimbali za wanamuziki wa Bongo Fleva, Lulu Eugen ‘Amber Lulu’ amelewa na sifa anazomwagiwa na ‘mpenzi’ wake mpya, Prezoo.
Amber Lulu alisema ana furaha ya ajabu kutokana na video aliyoiachia Prezoo akimsifia kwamba anampenda, ni mzuri na ana roho nzuri, achilia mbali kuwa ameshamt-ambulisha kwa mama yake.
“Najisikia vizuri sana kusifiwa na Prezoo maana mtu ukikubalika lazima ufurahi kwa kweli, ni mtu wangu wa karibu na tuna mpango wa kufanya kazi pamoja pia, kuhusu uchumba na kutambulishwa kwa mama yake hilo kwa sasa ni siri kidogo ila siku ikifika tutaweka wazi kila kitu,” alisema Amber Lulu.

NIYONZIMA:Yanga walipania sana
Kiungo wa Simba, Haruna Niyonzima, raia wa Rwanda.
KIUNGO wa Simba, Haruna Niyonzima, raia wa Rwanda, amekiri ugumu kukutana na timu yake ya zamani ya Yanga kutokana na wapinzani wake hao kumjua vilivyo.
Simba na Yanga zilikutana wikiendi iliyopita katika mchezo wa ligi kuu ambao ulikuwa na upinzani wa hali ya juu ambapo matokeo yalikuwa bao 1-1, huku Simba ikiendelea kuongoza katika msimamo kufuatia kuwa na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Wachezaji wa timu ya Yanga na Simba.
Akizungumza na Championi Jumatano , Niyonzima alisema, mchezo ulikuwa na upinzani mkubwa hivyo anashukuru kwa matokeo waliyoyapata na kudai ilikuwa kazi kwa upande wake kutokana na kucheza na timu yake ya zamani ambayo inamjua vilivyo, lakini ataendelea kupambana kuisaidia Simba.
“Mechi ilikuwa na ushindani, kila upande ulikuwa ukipigana kuweza kupata pointi tatu, lakini tunashukuru kwa matokeo haya tuliyoyapata, tunaamini mwalimu atafanyia kazi upungufu uliojitokeza ili tuweze kufanya vyema katika mechi zijazo.
“Mchezo ulikuwa mgumu, siyo kazi rahisi kwangu kupambana na timu niliyoichezea miaka mingi, pia wananifahamu, lakini nimejitahidi kucheza kulingana na jinsi hali ilivyokuwa, kwani nilikuwa na upinzani mkubwa, nilipambana kucheza katika kiwango kizuri kulingana na hali ilivyo ingawa walinisumbua sana,” alisema Niyonzima.

Tuesday, 31 October 2017

NDUGAI: SIJAPATA BARUA YA KUJIUZULU KWA NYALANDU, HUO NI UMBEA


SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, amesema kwamba hana taarifa za kujiuzulu kwa mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu na wala hiyo barua bado haijamfikia, amekiita kitendo alichokifanya ni umbea.
Job Ndugai ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na chombo kimoja cha habari nchini (jina tunalo) na kusema kwamba Lazaro hakupaswa kutangaza hivyo kabla ya kuhakikisha barua imemfikia.
Pamoja na hayo Spika Ndugai amewataka wabunge wengine kuacha kuwashwa washwa na kufanya mambo ambayo ameyaita ni ya umbea.

Source: globe publishers