Showing posts with label NEWS. Show all posts
Showing posts with label NEWS. Show all posts

Thursday, 18 August 2016

Ni kosa kumwangalia mwanamke kwa sekunde 14 nchini India

Watumiaji wa mitandao ya kijamii wamelalamika kuhusu tamko la afisa mmoja aliyesema kuwa ni kinyume na sheria kumuangalia mwanamke kwa zaidi ya sekunde 14 katika jimbo la Kerala nchini India.
http://hamisishehe.blogspot.com/2016/08/watumiaji-wa-mitandao-ya-kijamii.html
Hakuna sheria kama hiyo nchini India lakini afisa huyo Rishiraj Singh ambaye ni kamshna amesema kuwa kumuangalia mwanamke kwa mda mrefu kunaweza kukutia mashakani.
Watu mitandaoni wanauliza itakuwaje iwapo mwanamume atafunga jicho mara moja na kulifungua akimwangalia mwanamke wakiongezea kuwa huenda bei ya miwani ya kujilinda dhidi ya jua ikapanda.
Lakini wengine wanasema kuwa bwana Signh amezua hoja nzuri sana kuhusu usalama wa wanawake.
”Mtu anaweza kushtakiwa kwa kumuangalia mwanamke kwa sekunde 14”,alisema bwana Singh katika eneo la Kochi siku ya Jumamosi.
Tamko hilo lililofanywa katika kanda ya video limesambaa katika jimbo hilo na kuzua ucheshi miongoni mwa mitandao ya kijamii.
Source:BBC

Hili ndilo jina la ngoma mpya ya Alikiba?

Baada ya kuonjesha kile ambacho tutakiona kwenye video ya ngoma yake mpya, Alikiba anaweza akawa ametupa jina la wimbo huo.


http://hamisishehe.blogspot.com/2016/08/hili-ndilo-jina-la-ngoma-mpya-ya-alikiba.html
Add caption
Alikiba akiwa na warembo watakaoonekana kwenye video ya ngoma yake mpya
Mkali huyo wa Aje, ameanza kutumia neno #Kajiandae kwenye post zake mpya, huku kukiwa na uwezekano mkubwa kuwa likawa ndio jina la ngoma hiyo.
Hata hivyo bado haijulikani iwapo Kiba alienda Afrika Kusini kushoot video mbili au moja kwasababu hivi karibuni alidai kuwa alishoot video ya version ya Aje akiwa na rapper wa Nigeria, M.I.
Yeye pamoja na msanii mwenzake wa Rockstar4000, Barakah Da Prince walikuwa nchini humo kushoot video zao mpya

Wednesday, 17 August 2016

Darassa adai video ya ‘Too Much’ ilimtoa jasho

Rapper ambaye anafanya vizuri kwa sasa na ngoma yake, ‘Too Much’ Darassa, amesema video ya wimbo huo ilimtoa jasho


http://hamisishehe.blogspot.comAkiongea na kipindi cha Funiko Base cha Radio 5, Darassa alisema imemchukua muda mwingi na pesa nyingi kuikamilisha video hiyo kwakuwa alitaka kufanya kitu kikubwa.
“Too Much kwangu ni video kubwa na imetucost,imetuchukua muda,imetuumiza hapa ninavyoongea hakuna tulichobakiwa nacho zaidi ya nguvu na akili tu,” alisema.
“Tulichokuwa tunataka ni kuhakikisha tunatengeneza video nzuri nyumbani hata tukifanikiwa kimataifa watu wajue jamaa ameendelea tu ila alianzia nyumbani ndio tunachopambania,watu wa nje wahitaji kufanya kazi na sisi.”
Video ya wimbo huo iliongozwa na Hanscana.

Timbulo aitaja sababu ya kufuta sauti ya Malaika kwenye wimbo wake mpya

Msanii Timbulo amefunguka sababu iliyomfanya afute sauti ya Malaika na kumweka Nay Lee kwenye wimbo wake mpya wa ‘Ngomani’.

http://hamisishehe.blogspot.com
 
Muimbaji huyo amesema kuwa sababu kubwa iliyosababisha ni kuwa busy kwa Malaika kwa madai ya kutoweza kutokea kwenye video ya wimbo huo kwa sababu zake binafsi.
“Nilimshirikisha Malaika kwenye audio na alifanya vizuri lakini baadaye ilipofika muda wa kushoot video lakini siku hiyo akasema hatoweza kuja kwa sababu zake private,” amemuambia mtangazaji wa Fadhila FM ya Masasi, Dj Magasha.
“Video ilikuwa inahusisha watu wengi na tusingeweza kuisitisha kwa ajili yake tukaamua kumtafuta mtu mwingine aliyefiti kwenye hiyo ambaye ni Nay Lee,” ameongeza.
Aidha Timbulo ameendelea kwa kusema kuwa baada ya kumaliza kushoot video hiyo walirudi studio na wakaamua kuifuta sauti ya Malaika iliyokuwa kwenye wimbo huo na kuingiza upya sauti ya Nay Lee kwa sababu alifanya vizuri zaidi.

Zari awapa makavu wabaya wake

Ni muda mrefu mahusiano ya Diamond na Zari yameelezwa kutokuwa mazuri kutokana na muimbaji huyo kuhusishwa kutoka na warembo wengine.


hamisishehe


Kuna tetesi nyingi sana zimevuma kwenye mitandao ya kijamii hivi karibuni zikiwahusu Diamond na Zari.
Huku tetesi hizo zikimhusisha Diamond kusaliti mahusiano yake kwa kutoka na warembo wengine akiwemo Hamisa Mobetto na mrembo aliyetumika kwenye video ya wimbo wa ‘Kwetu’, Irene.
Kupitia mtandao wa instagram wa Zari ameandika ujumbe unaoonekana kuwalenga watu wanaomfuatilia na wasioyatakia mema mahusiano yao. “When your self made, it’s hard to break you no matter how hard they may try. I made me and the only person that can break me is ME not anybody. Ladies now wear this crown👑 and put them heels👠 on and keep it moving. Good night😘,” ameandika Zari.
hamisishehe
Hata hivyo wawili hao wanatarajia kupata mtoto pili wa kiume muda wowote kuanzia mwezi Disemba mwaka huu.

Wizkid kutumbuiza kwenye Fiesta ya Mwanza Jumamosi hii

Staa wa Nigeria, Wizkid, amethibitishwa kuwa atatumbuiza kwenye show ya Fiesta, Mwanza mwishoni mwa wiki hii.


Clouds FM wamethibitisha kumdondosha hitmaker huyo wa ‘Shabba’ Jumamosi, August 20.
“Kituuuuuuu #DealDone kwa mara ya kwanza ndani ya Mwanza #StarBoY wako @wizkidayo utatapata kumshuhudia LIVE juu ya jukwaa la #Fiesta2016 #Imooooo,” wameandika Clouds.
Hii itakuwa mara ya pili muimbaji huyo anakuja Tanzania. Mwezi October mwaka jana alitumbuiza kwenye viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam

source:bongo5