Saturday 13 August 2016

Maamuzi Magumu Aliyoyafanya Mzee Yusuf, Aachana na Uimbaji wa Taarab


TAARIFA hii ikufikie popote ulipo wewe mpenzi wa mziki wa taarabu na shabiki wa Mzee Yusuf. Gwiji wa mziki wa taarabu nchini Mzee Yusuf ‘Mfalme wa Taarab’ amethibitisha kuwa ameachana na kazi hiyo takribani miezi miwili iliyopita.
Taarifa zilizoenea katika mitandao ya kijamii hasa kuanzia jana zimeeleza kuwa mwanamziki huyo ameachana na mziki na kuamua kumrudia Mungu.
Akizungumza, mmiliki huyo wa bendi ya Jahazi Modern Taarab amethibitisha kuwa taarifa hizo ni za kweli: “Nashangaa taarifa hizi zinasemwa leo. Ni suala la muda mrefu… takribani miezi miwili iliyopita na sababu ni kuwa nimeamua kumrudia Allah,” Mzee Yusuf alisema.
Mwimbaji huyo wa huyo wa taarabu mzaliwa wa Zanzibar alipoulizwa kuwa ni suala gani lililomsukuma hata achukue maamuzi hayo magumu, alijibu kwa kifupi, “ndivyo tunavyofundishwa na viongozi wa dini.”
Yusuph aliyetamba na vibwagizo kama “Nichumu, nikisi….mwaaaa,” katika baadhi ya nyimbo zake, amesema familia yake imeupokea uamuzi wake kwa mtazamo chanya na kwamba inamuunga mkono.
“Kwa sasa nitaimba kaswida zenye mafundisho ya dini,” amesema nyota huo huku akiahidi kufanya mkutano rasmi kuelezea suala hilo.
Mfalme huyo aliyeonekana kuwa ni gwiji wa taarabu ya kisasa (modern taarab) amezaliwa visiwani Zanzibar mwaka 1977. Aidha amejihusisha na sanaa nyingine kama maigizo.
Ni mshindi wa tuzo katika tasnia ya muziki wa taarab zikiwemo ya Kilimanjaro Music Award 2014-15.
  1. Kikundi bora cha mwaka taarab – Jahazi Modern Taarab
  2. Mtunzi bora wa mwaka taarab- Mzee Yussuf
  3. Mwimbaji bora wa kiume taarab – Mzee Yussuf

Related Posts

Maamuzi Magumu Aliyoyafanya Mzee Yusuf, Aachana na Uimbaji wa Taarab
4/ 5
Oleh

Subscribe via email

Like the post above? Please subscribe to the latest posts directly via email.