Saturday, 13 August 2016

Ujauzito wa Zari nje nje, Diamond aomba ushauri jina la mtoto

Diamond atafuta jina la mtoto wake wa kiume baada ya mapema mwezi huu mkali huyo kuthibitisha ujio wa mtoto wake wa pili kutoka kwa mpenzi wake Zari.

Muimbaji huyo alidai kuwa mwezi Disemba mwaka huu anatarajia kupata mtoto huyo wa kiume, lakini baada ya hapo hatakuwa na mpango wa kuongeza mtoto mwingine.
Kwa sasa Diamond ameonekana kutafakari jina la kumpatia mtoto wake huyo mtarajiwa baada ya kutumia mtandao wa Instagram kumwandikia ujumbe mpenzi wake Zari ampatie jina la mtoto wao huyo.
Looking so sexy, my Beautiful and cute Wife @zarithebosslady😚 💞!!!… Please tell what would you like me to name my Upcoming Son?…
(Tafadhali niambie Mtoto wangu wa kiume unadhani akija nimwite jina gani…?)
 Na sasa mimba ya Zari inaonekana wazi baada ya kushare picha kadhaa kwenye Instagram.Diamond na Zari tayari wana mtoto mmoja wa kike, ‘Tiffa’ ambaye hivi karibuni ametimiza mwaka mmoja.

Related Posts

Ujauzito wa Zari nje nje, Diamond aomba ushauri jina la mtoto
4/ 5
Oleh

Subscribe via email

Like the post above? Please subscribe to the latest posts directly via email.