Tuesday, 16 August 2016

Nay wa Mitego adai Mr Ttouch anamchukulia kama mtoto aliyefikia umri wa kuondoka nyumbani

Rapper Nay wa Mitego amefunguka na kuzungumza madai ya kugombana na kuachana na mtayarishaji wake mahiri wa studio yake ya Free Nation, Mr Ttouch.Wawili hao kwa sasa kila mmoja anafanya kazi kivyake baada ya kudaiwa kuhitilafiana kwenye masuwala ya pesa.
Akiongea na Bongo5 Jumatatu hii, Nay wa Mitego amesema yeye hajagombana na Mr Ttouch kama baadhi ya watu wanavyosema.
“Mimi kwangu namchukulia Mr T kama mtoto aliyekuwa nyumbani na sasa amekuwa mtu mzima anaamua kutafuta maisha yake, kwa hiyo mimi namtakia mafanikio mema katika maisha yake,” alisema Nay.
“Mimi ndiye niliyemtafuta Mr T na kuamua kumkabidhi studio, nikawa sichukui hata shilingi mia, kwa hiyo mimi nachoweza kusema muache aende kwa sababu amekuwa mtu mzima,” aliongeza.
Pia rapper huyo amesema kwa sasa kama ana kazi atamtafuta mtayarishi huyo kwa ajili ya kazi lakini hawezi tena kufanya naye kazi kishkaji kama zamani.

Related Posts

Nay wa Mitego adai Mr Ttouch anamchukulia kama mtoto aliyefikia umri wa kuondoka nyumbani
4/ 5
Oleh

Subscribe via email

Like the post above? Please subscribe to the latest posts directly via email.