Thursday, 11 August 2016

Mimi ni Mungu wa bongofleva – Q Chief

Msanii mkongwe wa muziki, Q Chief amefunguka kwa kusema kuwa yeye ni Mungu wa muziki wa bongofleva kutokana na mambo makubwa alioyafanya kwenye muziki huo.


Muimbaji huyo aliyewai kutamba na nyimbo kama ‘Si Ulinikataa’, ‘Uhali Gani’ na nyingine, amekiambia kipindi cha Enewz cha EATV kuwa yeye ni Mungu wa bongofleva.
“Hii video yangu mpya ‘itaprove’ kwamba mimi ndiyo Mungu wa bongofleva,” alisema Q Chief. “Kuna wafalme, kuna chui, kuna simba, kuna paka, kuna mende lakini mimi siwezi kuwa wao, mi ni Mungu wa bongofleva,”
Aliongeza, “Nina miaka 15 kwenye game, nimepitia changamoto nyingi, nimepitia vipindi vingi, nimejifunza mambo mengi, baraka nilizokuwa nazo kupitia Mwenyezi Mungu huyu mmoja ambae tunamwabudu, nimeweza kupata kaka, rafiki, ngudu ambae ameona umuhimu wangu kwenye hili game,”
Muimbaji huyo anajipanga kuachia video yake mpya ya wimbo ‘Sungura’ aliyoshoot Afrika Kusini na Justin Campos.

Related Posts

Mimi ni Mungu wa bongofleva – Q Chief
4/ 5
Oleh

Subscribe via email

Like the post above? Please subscribe to the latest posts directly via email.