Showing posts with label SPORTS. Show all posts
Showing posts with label SPORTS. Show all posts

Wednesday 1 November 2017

NIYONZIMA:Yanga walipania sana




Kiungo wa Simba, Haruna Niyonzima, raia wa Rwanda.
KIUNGO wa Simba, Haruna Niyonzima, raia wa Rwanda, amekiri ugumu kukutana na timu yake ya zamani ya Yanga kutokana na wapinzani wake hao kumjua vilivyo.
Simba na Yanga zilikutana wikiendi iliyopita katika mchezo wa ligi kuu ambao ulikuwa na upinzani wa hali ya juu ambapo matokeo yalikuwa bao 1-1, huku Simba ikiendelea kuongoza katika msimamo kufuatia kuwa na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Wachezaji wa timu ya Yanga na Simba.
Akizungumza na Championi Jumatano , Niyonzima alisema, mchezo ulikuwa na upinzani mkubwa hivyo anashukuru kwa matokeo waliyoyapata na kudai ilikuwa kazi kwa upande wake kutokana na kucheza na timu yake ya zamani ambayo inamjua vilivyo, lakini ataendelea kupambana kuisaidia Simba.
“Mechi ilikuwa na ushindani, kila upande ulikuwa ukipigana kuweza kupata pointi tatu, lakini tunashukuru kwa matokeo haya tuliyoyapata, tunaamini mwalimu atafanyia kazi upungufu uliojitokeza ili tuweze kufanya vyema katika mechi zijazo.
“Mchezo ulikuwa mgumu, siyo kazi rahisi kwangu kupambana na timu niliyoichezea miaka mingi, pia wananifahamu, lakini nimejitahidi kucheza kulingana na jinsi hali ilivyokuwa, kwani nilikuwa na upinzani mkubwa, nilipambana kucheza katika kiwango kizuri kulingana na hali ilivyo ingawa walinisumbua sana,” alisema Niyonzima.

Friday 12 August 2016

Mavugo: "Tambwe kwangu ni cha mtoto tu"



Nyota huyo mpya aliyesaini mkataba wa miaka miwili ametamba kuwa yeye ni tishio kuliko Amissi Tambwe ambaye ni maarufu kwa kucheka na nyavu
Mshambuliaji mpya wa Simba, Laudit Mavugo amesema amejipanga kuifanyia mambo makubwa klabu hiyo kumzidi Mrundi mwenzake Amissi Tambwe anayeichezea Yanga.

Mavugo ameiambia Goal, amepata taarifa kuwa Tambwe ndiye mshambuliaji, anayeogopewa kwenye ligi ya Tanzania kwa ufungaji, na kusema ametua kwa ajili ya kumpoteza mshambuliaji huyo aliyewahi kuwa mfungaji bora wa ligi ya Vodacom mara mbili akiwa na timu za Simba na Yanga.

“Namfahamu Tambwe ni mchezaji mwenzangu wa timu ya taifa ya Burundi ‘Intamba murugamba’ lakini uwezo wake wa ufungaji bado hajanifikia naahidi kumpoteza katika kipindi cha misimu miwili ambayo nimesaini hapa,” amesema Mavugo.

Mshambuliaji huyo aliyefunga bao moja kwenye mchezo wake wa kwanza kuichezea Simba, amekuwa tumaini kubwa la mashabiki wa Simba kufuatia kuonyesha kiwango bora katika mchezo wake wa kwanza wa utambulisho.

SOURCE:GOAL