Wednesday, 17 August 2016

Sare za polisi zawaponza wasanii wa Orijino Komedi, kuburuzwa Mahakamani

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam kuwachukulia hatua wasanii wa Kundi la Orijino Komedi kwa kuvaa mavazi yanayoshabihiana na sare za polisi.


Akiongea na Clouds FM Msemaji wa Polisi, Advera Bulimba ameeleza kuwa wanatoa onyo kali kwa mtu ama kikundi chochote kuacha kutumia mavazi yanayofanana na sare zinazovaliwa na majeshi ya ulinzi na usalama hapa nchini na atakayebainika hawatasita kuchukua hatua kali za kisheria dhidi yake.
“Jeshi la Polisi linawashikilia wasanii wa Kikundi cha Orijino Komedi kwa kuvaa sere za polisi, hilo moja kwa moja ni kosa kisheria na tayari Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam limechukua hatua ya kuwakamata baada ya kukamilisha taratibu zote za kisheria wasanii hao watafikishwa Mahakamani. Kufanya hivyo ni kosa, na watuhumiwa wanatakiwa washughulikiwe kwa mujibu wa sheria za nchi yetu,” alisema Advera.
Wasanii hao wa Kundi la Orijino Komedi walivaa sare hizo katika harusi ya mchekeshaji mwezano Masanja Mkandanizaji.

source:bongo5

Related Posts

Sare za polisi zawaponza wasanii wa Orijino Komedi, kuburuzwa Mahakamani
4/ 5
Oleh

Subscribe via email

Like the post above? Please subscribe to the latest posts directly via email.