Friday, 12 August 2016

Mavugo: "Tambwe kwangu ni cha mtoto tu"Nyota huyo mpya aliyesaini mkataba wa miaka miwili ametamba kuwa yeye ni tishio kuliko Amissi Tambwe ambaye ni maarufu kwa kucheka na nyavu
Mshambuliaji mpya wa Simba, Laudit Mavugo amesema amejipanga kuifanyia mambo makubwa klabu hiyo kumzidi Mrundi mwenzake Amissi Tambwe anayeichezea Yanga.

Mavugo ameiambia Goal, amepata taarifa kuwa Tambwe ndiye mshambuliaji, anayeogopewa kwenye ligi ya Tanzania kwa ufungaji, na kusema ametua kwa ajili ya kumpoteza mshambuliaji huyo aliyewahi kuwa mfungaji bora wa ligi ya Vodacom mara mbili akiwa na timu za Simba na Yanga.

“Namfahamu Tambwe ni mchezaji mwenzangu wa timu ya taifa ya Burundi ‘Intamba murugamba’ lakini uwezo wake wa ufungaji bado hajanifikia naahidi kumpoteza katika kipindi cha misimu miwili ambayo nimesaini hapa,” amesema Mavugo.

Mshambuliaji huyo aliyefunga bao moja kwenye mchezo wake wa kwanza kuichezea Simba, amekuwa tumaini kubwa la mashabiki wa Simba kufuatia kuonyesha kiwango bora katika mchezo wake wa kwanza wa utambulisho.

SOURCE:GOAL

Related Posts

Mavugo: "Tambwe kwangu ni cha mtoto tu"
4/ 5
Oleh

Subscribe via email

Like the post above? Please subscribe to the latest posts directly via email.