Thursday, 11 August 2016

"mauno yangu Yamechangia Kunikuza Kimuziki"-Snura
Msanii Snura ambaye mara nyingi amekuwa akikumbwa na rungu la BASATA kutokana na video zake ambazo zinakuwa na utata, amesema mauno ambayo BASATA 'wanamind' ndio yamemfikisha hapo alipo.

Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Snura amesema mauno yake ndiyo yamechangia kwa kiasi kikubwa kuinua muziki wake, kutokana na jinsi anavyoyamwaga akiwa jukwaani, na kuwavutia mashabiki wake.

"Nimeimba sana laini kiuno changu kimenisaidia sana kunitambulisha, ukisikia kuna show ya Snura jua mauno yanamwagwa kweli, na sijaanza leo nilianzia kwenye ngoma za asili", alisema Snura.
Snura aliendelea kusema kuwa ingawa mauno hayo humpa wakati mgumu akiwa kwenye kazi zake kutokana na uchu wa baadhi ya wanaume wanaomsumbua, lakini amekuwa akijitahidi sana kujilinda ili asiharibu kazi yake.

"Usumbufu kiukweli upo,wengine wananipenda kweli wengine wananitamani, kikubwa nazingatia sana kazi yangu, nashinda sana vishawishi kwa sababu vile ninavyokatika wengine wanadhani nafanya promotion ya biashara", alisema Snura.

Related Posts

"mauno yangu Yamechangia Kunikuza Kimuziki"-Snura
4/ 5
Oleh

Subscribe via email

Like the post above? Please subscribe to the latest posts directly via email.