Thursday, 11 August 2016

Kilichowatibua The Rock na Vin Diesel kwenye utengenezaji wa Fast 8 chafahamika

Waigizaji wa filamu ya Fast and Furious 8, Dwayne “The Rock” Johnson na Vin Diesel walivimbiana hivi karibuni kiasi cha kukaribia kuzichapa live


Hali hiyo ilimpelekea The Rock kulalamika kwenye Instagram akiwashutumu baadhi ya waigizaji wa kiume wa filamu hiyo kuwa wana mambo ya kimbwiga na baadaye kufahamika madongo hayo yalimhusu Diesel.
Na sasa tovuti ya Page Six imeeleza sababu za mafahari hao kuchemshana damu.
“Vin Diesel na Dwayne Johnson wamekuwa wakikorofishana muda wote kwenye utengenezaji wa ‘Fast 8,’” chanzo kimoja kiliiambia Page Six. “Vin ana sifa ya kuwa pasua kichwa, huchelewa kufika, huwafanya watu wamngoje, husimamisha utengenezaji na huwa hawaheshimu watu kwenye utengenezaji. Uvumilivu ulimshinda Dwayne.”
Chanzo hicho kiliongeza, “walikuwa na mkutano wa kujaribu kuyamaliza Jumanne. Jumatano, Diesel alimaliza kufanya scene yake ya mwisho na Johnson alidaiwa kumaliza sehemu yake kwenye filamu hiyo baadaye.”
Diesel pia ni producer wa filamu hiyo huku TMZ ikidai kuwa The Rock hakufurahishwa na baadhi ya maamuzi aliyoyafanya wakiwa location.
Diesel amekuwa na sifa ya usumbufu Hollywood. Chanzo kimoja kilichowahi kufanya naye kazi kimedai: Alikuwa akichelewa muda wote, alikuwa akifanya mambo kama mwanamke na aliwahi kuchelewesha utengenezaji kabla, hivyo sishangai kuwa ndiye ambaye The Rock amemchana.”
Lakini vyanzo vingine vimedai kuwa ni The Rock ndiye amekuwa akichelewa kwenye utengenezaji wa filamu hiyo kiasi cha kumtibua Diesel.
Kwenye Instagram, The Rock aliandika: My female co-stars are always amazing… My male co-stars however are a different story. Some conduct themselves as stand up men and true professionals… The ones that don’t are too chicken s–t to do anything about it anyway. Candy asses.”

Related Posts

Kilichowatibua The Rock na Vin Diesel kwenye utengenezaji wa Fast 8 chafahamika
4/ 5
Oleh

Subscribe via email

Like the post above? Please subscribe to the latest posts directly via email.