Thursday 11 August 2016

Hirizi Ya Tiffah Yaibua Jipya...


Mtoto wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Tiffah Dangote Agosti 3, mwaka huu ametimiza mwaka mmoja lakini jipya lililoibuka ni kuhusiana na dawa ‘hirizi’ aliyovalishwa mkononi na bibi yake mzaa baba, Sanura Kassim ‘Sandra’, Risasi limenyetishiwa ubuyu.

Chanzo kutoka ndani ya familia ya mastaa hao kilichoomba hifadhi ya jina lake kimedai kuwa, awali Tiffah alivishwa dawa hiyo lengo likiwa ni kumkinga na matatizo lakini Zari alipokwenda Sauzi akamvua kwa kuwa yeye si ‘muumini’ wa mambo hayo.

tiffaIkadaiwa kuwa, baada ya Zari kumvua walikaa muda mrefu bila Tiffah kuwa na ‘kadawa’ hako hali iliyomfanya mtoto huyo achelewe kutembea.

“Unajua ile dawa ina mambo mengi kwa watoto, inamsaidia kumkinga na matatizo lakini pia inamfanya atembee haraka, sasa walipoivua ikamfanya achelewe kutembea,” alisema mtoa habari huyo na kuongeza:

“Hali hiyo ilisababisha Zari na Diamond kutofautiana na mwisho wakakubaliana hirizi irejeshwe mkononi mwa Tiffah ndipo mtoto huyo alipoanza kutembea.”

Ikaelezwa kuwa, kuanza kutembea kwa Tiffah kumeibua furaha upya kwenye familia hiyo kwani walishaanza kuwa na hofu hasa ikichukuliwa kuwa, Zari ana mimba nyingine na anatarajiwa kujifungua Desemba, mwaka huu.

Kufuatia madai hayo, mwandishi wetu alimtafuta Diamond na alipopatikana alisema kuwa ni kweli mtoto wao ameanza kutembea lakini si kwa sababu ya dawa hiyo aliyofungwa mkononi.

“Hayo mambo ya kumvalisha na kumvua Tiffah ile dawa ya mkononi ni uamuzi tu lakini huwezi kusema ina uhusiano na kutembea kwake,” alisema Diamond.

Source:GPL

Related Posts

Hirizi Ya Tiffah Yaibua Jipya...
4/ 5
Oleh

Subscribe via email

Like the post above? Please subscribe to the latest posts directly via email.