Thursday, 11 August 2016

Diamond kutoa zawadi ya Tsh 5M kwa kikundi kitachoweza kudansi style ya wimbo ‘Kidogo’

Diamond Platnumz baada ya video yake ya wimbo ‘Kidogo’ kufikisha views milioni 3 ndani ya mwezi mmoja, ametangaza kutoa zawadi ya tsh 5 milioni kwa kundi la vijana wataoweza kuonyesha uwezo mkubwa wa kudansi kupitia wimbo huo.


Muimbaji huyo amewataka madansa kuonyesha uwezo wao wa kudansi wimbo huo pamoja na kuchanganya na style mpya.
“Nipo na milioni 5 cash mkononi kwa kikundi kitachotuma clip ya kudansi ‘‪Kidogo’‬ sawia haswaaaa! yaani sio kiwasiwasi waue haswaaaa,” aliandika Dimaond kupitia instagram.
Aliongeza, “Tena wamix na style zao wenyewe. Narudia tena wauwe haswaaa!. haya wapigie simu wanao mjipange kesho tume clip kwa namba hii +255654019091 na mkisha tuma mpandishe insta na kuhashtag neno #Kidogo, na kesho hiyo ntatangaza mshindi anapatikanaje,”
Video ya wimbo ‘Kigogo’, ni video ya kwanza ya msanii wa Tanzania kufikisha views milioni 3 kwa kipindi cha mwezi mmoja.


Related Posts

Diamond kutoa zawadi ya Tsh 5M kwa kikundi kitachoweza kudansi style ya wimbo ‘Kidogo’
4/ 5
Oleh

Subscribe via email

Like the post above? Please subscribe to the latest posts directly via email.